Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jobe, Fredy ni wabovu

Jobe X Freddy Jobe, Fredy ni wabovu

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Simba SC, Mchome Mapovu amesema kuwa washambuliaji wapya wa timu hiyo, Pa Omar Jobe na Michael Fredy ni wabovu na hawana uwezo wa kuichezea timu hiyo kutokana na ukubwa wake.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons juzi katika uwanja wa CCM Jamhuri mjini Morogoro.

“Hakuna cha Jobe wala Fredy, wote ni washambuliaji wabovu, tunawashangilia kwa mechi moja moja tu lakini hawana mwendelezo. Angalau Jobe anaonesha ana kitu anapambana pambana lakini kufunga hajui.

“Fredy najiuliza mpaka sasa Simba anafanya nini, hajui kitu. Bora ucheze na false number 9 Kibu lakini sio yule mchezaji.

“Mechi muhimu Benchikha anmwanzisha yule jamaa, hizi sio mechi za kupima mchezaji, umeachwa alama saba huwezi kusema unakimbiza ubingwa, hatupo siriazi,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: