Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Simba kuweni 'serious'

Simba Power Ms.jpeg Jemedari Said: Simba kuweni 'serious'

Mon, 18 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini kupitia EFM, Jemedari Said Bin Kazumari amewataka Klabu ya Simba kuwa 'serious' kwenye michezo yao ya kimataifa, la sivyo watapoteza michezo yao ijayo.

Kauli hiyo ya Jemedari inakuja baada ya Simba kutoa sare ya bao 2-2 dhidi ya Power Dynamos ya Zambia juzi Jumamosi, Septemba 16, 2023 wakati wa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa katika Dimba la Levy Mwanawasa nchini humo.

"Hawa Simba wanapaswa kujua kuwa Kuna jukumu zito mbele yao kwenye Hatua ya Makundi na African Super League, namna jana walivyocheza haikuvutia wengi ingawa hatua hizi lengo huwa kuvuka na sio kuvutia.

"Wanapaswa kutumia nafasi zinazotengenezwa kwakuwa mechi kubwa kubwa nafasi ni chache, lengo la nusu fainali linahitaji matumizi sahihi ya nafasi," amesema Jemedari Said.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: