Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari Said: Simba iheshimiwe, Robertinho aachwe afanye kazi

Jemedari Said The Voice Less Jemedari Said

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba SC ikiondoshwa katika michuano ya African Football League na Al Ahly kwa faida ya bao la ugenini.

Mchambuzi wa Soka kutoka kituo cha Efm, Jemedari Said ameandika andiko katika ukurasa wake wa Instagram akiwataka wapenzi na Mashabiki wa soka nchini kuona lile kubwa lililofanywa na Simba badala ya kuanza kuwadhihaki.

Jemedari ameandika;

"Kanuni ya bao la ugenini imeiondoa Simba SC kutoka kwenye mashindano ya African Football League (AFL). Baada ya sare ya nyumbani ya 2-2 Leo imetoka sare nyingine ya ugenini ya 1-1 pale Cairo Misri dhidi ya Ahly. Sio kila timu inaweza kuidindia Ahly namna hii hasa ukanda huu wa CECAFA, Ahly ndio klabu ya Karne, ndiyo klabu ya kihistoria Afrika, klabu namba 1 kwa ubora Afrika kwa sasa, ndiyo Mabingwa watetezi wa CAF CL wakishinda mara 11 ambayo ni rekodi

Haikuwa rahisi kwenye mechi zote 2 Simba wameonyesha kwanini wao walistahili kuwapo AFL kutoka CECAFA na sio timu nyingine, wameonyesha kwanini wao ni klabu bora Tanzania na CECAFA yote kwa miaka 5 mfululizo.

There is always next time boys, you fought a lot but wasn’t your luck, heads up"

Je unadhani Simba wanastahili heshima? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: