Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jemedari: Okwa amekuwa mkweli

Nelson Okwa Ulaya Nleson Okwa.

Wed, 28 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Jemedari Said amesema kuwa aliyekuwa kiungo wa Simba, Nelson Okwa amekuwa mkweli kuhusu figisu alizokuwa akifanyiwa ndani ya Simba hali iliyosababisha kuondoka klabuni hapo.

Jemedari amesema kuwa wachezaji wengi wanaumia lakini wanaogopa kusema ukweli hivyo kuwafanya kushuka viwango sababu ya kutopangwa kucheza.

"Mchezaji ukisajiliwa kwenye timu unakua na matumaini makubwa sana moja wapo ikiwa ni kupata nafasi ya kucheza kuonyesha kipaji chako.

"Unakua na malengo yako binafsi pia ambayo unayapanga na la kwanza ni kupata nafasi ya kucheza, kisha yatafuata mengine ambayo yanatokana na kucheza tena kucheza vizuri.

"Katika makosa makocha wetu wanafanya ni kutokuongea na wachezaji hasa wasiopata nafasi ya kucheza ili kuwajenga kwa kuwaambia makosa yao, kwanini hawachezi, nini wafanye nk.

"Okwa kama binadamu na mchezaji ana haki ya kufanya mahojiano na vyombo vya habari, ni haki yake kabisa ya msingi. Kwangu mimi aliyoongea mengi yanafanyika kwenye vilabu vyetu vyote na mimi naweza kuwa shuhuda katika hili.

"Tofauti ni kwamba Okwa amekuwa mkweli kuyasema leo, lakini wachezaji wengi wanaishi na maumivu tele mioyoni mwao iwe wa nje au hapa ndani ni vile hawajaamua kusema kwa sababu zao," amesema Jemedari..

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: