Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jembe: Mkude awafanyie sherehe Simba, wamemvumilia sana

Mkude Pic Data Jonas Mkude

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi mahiri wa soka, Saleh Ally Jembe amesema Klabu ya Simba imemvumilia sana aliyekuwa mchezaji wake, Jonas Mkude kutokana na matukio mbalimbali ya utovu wa nidhamu aliyokuwa akiyafanya.

Jembe amesema kuwa hata ikitokea Mkude ameenda Yanga, kwake anaona ni sawa kwa sababu mchezaji anao uhuru wa kuchagua timu anayoitaka lakini akatahadharisha kwamba anatakiwa kujirekebisha kwa sababu siyo klabu zote zinazoweza kuvumilia matatizo yake.

“Mkude kwenda Yanga au asiende huo ni uamuzi wake, ana haki ya kucgaua pa kwenda, cha pili nisema Simba hawapaswi kujuta kumpoteza Mkude kwa kuhofia mashabiki.

“Ukiwa kiongozi ukawa unahofia mashabiki, basi unatoka kwenye sifa za kuwa kiongozi bora, badala yake kiongozi unatakiwa uangalie usahihi wa jambo unaloliamua hata kama watu wote hawakuungi mkono.

“Ukiangalia kwa misimu miwili msaada wa Mkude kwa Simba ulikuwa chini sana, na sisi waandishi wa habari tunajua na tumesikia mambo mengi ya ndani ambayo ukiangalia klabu ndiyo ilikuwa ikimvumilia mkude.

“Nashangaa watu wanasema kwa nini Mkude hajaagwa? Unajiuliza kwa kipindi hiki (likizo ya msimu) Simba waandae mechi wakusanye wachezaji kwa ajili ya kufanya sherehe ya kumuaga Mkude? Hilo nadhani litafanyika kwenye Simba Day.

“Lakini najiuliza kwa nini Mkude naye asiwafanyie sherehe Simba? Kwa sababu walimlea, wakamvumilia kwa mambo mengi sana. Mkude akienda Yanga hakuna shida yoyote, lazima kuna vitu atatakiwa abadilike, maana si kila mtu atamvumilia tabia yake,” amesema Jembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: