Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Jean Baleke amnyima usingizi Kocha Azam

Baleke Mchezaji Bora Jean Baleke

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha msaidizi wa Azam FC, Kally Ongala amedai kuwa wana presha kubwa baada ya idadi kubwa ya mabao yalifungwa na wachezaji wa Simba akiwemo mshambuliaji, Jean Baleke katika mchezo wa robo fainali ya Azam Sports Federetion Cup kukutana nao kwenye nusu fainali ya michuano hiyo.

Ijumaa ya wiki iliopita Simba ilifanikiwa kusonga mbele hatua ya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ihefu, wakati Azam walicheza na Mtibwa Sugar na kuibuka na ushundi wa 2-1 katika mechi zilizochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Azam FC watakutana na Simba katika hatua ya nusu fainali ya kombe hilo kwenye mchezo unaotarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Akizungumza nasi, Ongala alisema ushindi wa mabao mengi ya Simba katika mechi iliyopita imewapa presha kubwa na kurejea katika uwanja wa mazoezi kufanyia kazi madhaifu yao kabla ya mchezo wa nusu fainali ya kombe hilo.

“Ni kweli ushindi wa wenzetu (Simba) katika robo fainali umezidisha presha kubwa kwetu, kujipanga na kufanyia kazi mapungufu yetu na ubora wa Simba katika safu yao ya ushambuliaji inaonekana hatari.

“Nadhani tunatakiwa kujipanga vizuri kwa kuhakikisha tunatumia vyema mechi zetu za ligi kama sehemu ya maandalizi kuelekea mchezo wa nusu fainali kwa sababu malengo yetu ni kuona tunachukua ubingwa wa michuano hii,” alisema Ongala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: