Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inonga ashonwa nyuzi 13, aruhusiwa kutoka hospitali

Henock Inonga Baka Inonga ashonwa nyuzi 13, aruhusiwa kutoka hospitali

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mratibu wa Klabu ya Simba, Abbas Ally amezungumza akiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ambapo Beki, Henock Inonga Baka alifikishwa kwaajili ya matibabu baada ya kupata majera kwenye mchezo na Coastal Union yaliyopelekea kuchukuliwa na ambulance.

Abbas amesema kuwa Inonga anaendelea vizuri na ameruhusiwa kwenda nyumbani, kuhusu majeraha Mratibu huyo wa Klabu amesema vipimo vya X-rays vimeonesha jeraha limeishia kwenye ngozi halijafika kwenye mfupa ingawaje ameshonwa nyuzi nyingi.

"Beki wetu Inonga Kashonwa nyuzi 13 katika jeraha hilo na tayari amesharuhusiwa Kurudi nyumbani. Amepata jeraha palepale ambapo aliumia katika mchezo dhidi Tanzania Prison.

"Habari njema ni kwamba, Inonga hajavunjika mfupa bali ni kidonda tu, kuhusu kuwa atakuwa nje kwa mda gani inategemea na jinsi atakavyopona kidonda," amesema Abbas.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: