Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Inonga, Che Malone wapewa shoo, yaani mpaka mseme...

Inonga X Che Malone Mzuka Inonga na Che Malone.

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki yeyote asiyeipenda Simba anasubiri kuona bato la mshambuliaji wa Al Ahly, Percy Tau na ukuta wa Simba, lakini kocha wa Wekundu hao, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ameibuka na kutoa kauli nzito akisema wana chuma Che Malone Fondoh, mwenye uwezo wa juu kuliko hao Waarabu.

Hii ni sawa na kauli ya mjini inayotamba kwa sasa, Bado Hamjasema!!!

Mbali na Malone, ambaye anafahamika kama ukuta wa Yeriko, Simba wamekuwa na mabeki wazoefu ambao wanaweza kupambana na Al Ahly, yupo Inonga Bacca ambaye awali mashabiki walikuwa na wasiwasi, lakini sasa amerejea, lakini kuna Shomary Kapombe na Mohamed Hussein ambao wamewahi kuvaana na Waarabu hao mara kadhaa na kuibuka na ushindi.

Akizungumza nasi, Robertinho amesema hana presha na ukuta wa timu yake kwa kuwaangalia washambuliaji wa Ahly kwani kama kuna usajili bora ambao Simba wameufanya ni kumshusha Che Malone ambaye amethibitisha kuwa ni beki wa viwango vya juu.

Kocha huyo mwenye mbwembwe alisema Che Malone ambaye ametua Simba akitokea Cotton Sport ya Cameroon hawezi kushtuka kukutana na Ahly kwani msimu uliopita alishapambana nao sambamba na vigogo wa Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns tena ndani nje.

Amesema beki huyo ambaye yupo daraja sawa la ubora na Henock Inonga, kuanzia alipotua amethibitisha ubora wake akiisaidia Simba kushinda mechi zote tano za Ligi Kuu Bara na pia akiipeleka makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Nawaheshimu Al Ahly wana timu bora lakini mimi sio muumini kumsemea mchezaji mmojammoja, ni kweli wana washambuliaji bora lakini hata Simba tuna mabeki bora pia, angalia una wasiwasi gani unapokuwa na beki kama Che Malone?,”alihoji Robertinho.

“Che Malone ni beki bora wa viwango vya juu naweza kusema yuko daraja bora na Inonga, mnaweza kuangalia takwimu zake tangu amefika hapa Simba amekuwa kwenye kiwango kizuri sana na kuna wakati amekuwa na akili kubwa ya kwenda kuibeba timu inapofanya makosa.

“Ana uzoefu mkubwa watu wanatakiwa kuheshimu wakati Simba inamsajili alikuwa anatoka kupambana na Ahly pamoja na Mamelodi tena akianza michezo yote na kuonyesha ubora, hizi ni timu bora ndio maana Simba wakamsajili.

“Anajua kuwapanga wenzake uwanjani na kucheza kwa nidhamu kubwa kitu ambacho kinahitajika kwenye mechi kubwa kama hizi hivyo hatuna hofu,” alisema.

Robertinho alisema wamefanya na wanaendelea kufanya mazoezi mengi ili kuhakikisha ukuta wake unakuwa kwenye utulivu mkubwa kuelekea mechi hiyo ya kwanza ya ufunguzi wa African Football League dhidi ya Waarabu hao itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa Mkapa kuanzia saa 12:00 jioni.

Msimu uliopita Malone alikuwa Cotton Sports ambayo kwenye hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Afrika ilipangwa kundi moja na Ahly, Mamelodi na Al Hilal ya Sudani.

Katika kundi hilo, Mamelodi na Al Ahly ndizo zilikwenda hatua ya robo fainali ya mashindano hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: