Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu ndio pilato wa Simba, Yanga Kwa Mkapa kesho

Arajiga Ahmed (600 X 537) Arajiga pilato wa Simba, Yanga Kwa Mkapa kesho

Sat, 4 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati homa ya pambano la watani wa jadi ikianza kupanda kabla ya timu hizo kuvaana Jumapili ya kesho Novemba 5, Bodi ya Ligi imetaja waamuzi watakaopewa pambano hilo litakalopigwa Uwanja wa Mkapa saa 11:00 jioni.

Imezoeleka mara nyingi majina ya waamuzi wanaopewa pambano hilo hufichwa na kuja kutajwa siku moja kabla na leo Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Karimu Boimanda, amewataja waamuzi wane na Kamishna wa ‘Kariakoo Derby’

Ahmed Arajiga ataamua dabi hiyo kama muamuzi wa kati akiwa na wasaidizi Muhamed Mkono na Kassim Mpanga na wa akiba ni Ramdhani Kayoko huku Kamishana wa mchezo ni Hosea Lugano kutoka Lindi

Simba itaikaribisha Yanga ikiwa ni dabi yao ya pili msimu huu wa ligi baada ya ile ya Ngao ya Jamii iliyochezwa Agosti jijini Tanga, Simba ikibeba ngao hiyo

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: