Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu hapa mpinzani wa Simba Ligi ya Mabingwa Afrika

Simba Mazoezi Tr Wachezaji wa Simba SC wakijifua

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba SC kutoka Tanzania itaanzia hatua ya raundi ya pili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/24.

Simba wao watasubiri mshindi wa mechi kati ya African Stars ya Namibia dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

African Stars ndio Bingwa wa Ligi Kuu ya nchini Namibia msimu uliopita akinyakua ubingwa kwa uongozi wa alama 73 baaada ya Michezo 30 wakishinda michezo 22, sare 7 na kupoteza mchezo mmoja pekee.

Power Dynamos nao ni Mabingwa wa Ligi Kuu ya Zambia kwa msimu uliopita 2022/23 wakiibuka vinara kwa kujikusanyia alama 65 wakicheza michezo 34 ambapo walishinda michezo 17, sare michezo 14 huku wakipoteza michezo mitatu.

Mchezo wa Mkondo wa kwanza kati ya African Stars dhidi ya Power Dynamos utapigwa kati ya Agosti 18, 19 na 20, huku mkondo wa pili ukpigwa kati ya Agosti 25, 26 na 27.

Michezo ya raundi ya pili Simba wataanzia ugenini na mechi za Mkondo wa kwanza zitapigwa kati ya Septemba 15, 16 na 17 huku michezo ya Mkondo wa pili ikipigwa Septemba 29, 30 na Oktoba 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: