Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huyu Baleke balaa muda huu

Balekeee Simbas.jpeg Huyu Baleke balaa muda huu

Sun, 1 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Simba inashuka uwanjani jioni ya leo kuikabili Power Dynamos ya Zambia katika pambano la marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, huku rekodi zikionyesha, straika Jean Baleke ameonekana kuwa tishio hasa kipindi cha kwanza kwenye mechi alizocheza.

Baleke ndiye kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara na Simba kiujumla baada ya kufunga mabao matano hadi sasa.

Mshambuliaji huyu kutoka DR Congo, licha ya kutofunga bao katika mchezo wa kwanza za raundi ya pili ya CAF dhidi ya Dynamos uliomalizika 2-2 mjini Ndola, lakini kwenye Ligi amekuwa tishio. Mabao ya Simba kwenye mechi ya ugenini yote yalifungwa na Clatous Chama.

Baleke kwenye Ligi amefunga mabao yote matano ndani ya kipindi cha kwanza jambo ambalo kama akiendelea nalo kwenye mchezo huu wa marudiano dhidi ya Dynamos basi mechi itaisha kipindi cha kwanza.

Bao lake la kwanza msimu huu Baleke alifunga dakika ya tano tu katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao Simba ilishinda 4-2.

Bao la pili alifunga dakika ya 44 katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji wakati Simba ikishinda 2-0, huku mabao mengine matatu wakati akipiga hat trick dhidi ya Coastal Union kwnye ushindi wa 3-0, nyota huyo aliyemaliza na mabao tisa msimu uliopita katika ligi hiyo, pia aliyafunga ndani ya kipindi cha kwanza.

Mabao hayo aliyafunga dakika 7, 11 na 40 na kumpandisha hadi kileleni mwa orodha ya wafungaji wa msimu huu akimshusha Feisal Salum 'Fei Toto' aliyekuwa anaongoza kwa mabao matatu aliyofunga kwenye mechi ya kwanza ya Ligi msimu huu akiwa na Azam ilipoizamisha Tabora United iliyokuwa pungufu.

Kama moto alioanza nao Baleke utaendelea leo na kwenye mechi ijayo ya Ligi itakayopigwa ugenini jijini Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons, basi mshambuliaji huyo ataendelea kukimbiza.

Akizungumzia kiwango cha mshambuliaji huyo, Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ alisema anajivunia na mchezaji kama huyo katika kikosi chake.

Robertinho alisema Baleke anajua kutumia nafasi zinazopatikana na ndio maana anafunga kila inapokuwa inatokea.

“Hakuna shaka kwamba ni mshambuliaji mzuri ndani ya kikosi chetu, anajua kufunga kila nafasi inapotokea mbele yake na tunajivunia hilo. Sio yeye tu wapo wachezaji wengi ndani ya Simba kwa sasa wana vipaji vikubwa mno ambavyo vinavutia,” alisema Robertinho.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: