Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Huko Sokoine hakijaeleweka, mashabiki kiduchu

Mashabiki Sokoine Huko Sokoine hakijaeleweka, mashabiki kiduchu

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati wadau na mashabiki jijini Mbeya wakisubiri kwa hamu mchezo wa Ligi Kuu kati ya Prisons na Simba, idadi ya wanaoingia uwanjani imeonekana kupungua hadi sasa tofauti na inavyokuwa siku nyingine.

Mchezo huo wa raundi ya nne kwenye ligi hiyo unatarajia kuchezwa saa 10:00 jioni katika uwanja wa Sokoine jijini hapa kwa viingilio vya Sh5,000 (mzunguko) na Sh30,000 jukwaa kuu (VIP).

Tofauti na siku nyingine ambapo nje ya uwanja huwa kumefurika kwa muingiliano wa watu kuhangaika kutafuta tiketi au kuingia uwanjani, leo imekuwapo mabadiliko.

Juma Mweta mdau na shabiki wa soka jijini hapa amesema kutokana na kuwa siku ya kazi, huenda wadau wakajitokeza baadaye kwani kwa sasa wanahangaika kutafuta kwanza riziki.

“Lazima ujue leo ni siku gani, watu muda huu wanaendelea na majukumu yao maofisini kutafuta riziki, hata idadi hii iliyopo kwa sasa si haba,”

Naye Tatu Samuel amesema kutokana na mechi kupigwa jioni, huenda idadi ikaongezeka kwani uwanja unaotumika upo katikati ya jiji hivyo walipo maofisini hawatakuwa na tatizo.

“Uzuri uwanja upo mjini naamini watakaotoka mapema kazini wataingia ndani, muda haujaisha, ila naitakia Simba ushindi ili tupande kileleni,” alisema Tatu shabiki wa Wekundu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: