Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndo tofauti ya mashabiki wa mpira na wanywa supu za vibudu - Ahmed

Ahmed All Supu Day Hii ndo tofauti ya mashabiki wa mpira na wanywa supu za vibudu - Ahmed

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Mashabiki wa Simba kutangazwa kuwa mashabiki bora wa AFL 2023, Afisa habari wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema kuwa hiyo ni heshima kuliko mashabiki wanywa supu.

Dongo hilo linakwenda moja kwa moja kwa wapinzani wao Yanga ambao Jumapili iliyopita walijipongeza kwa kunywa supu baada ya kuwafunga Simba bao 5-1, Novemba 5, 2023.

“Tumeshinda tuzo ya mashabiki bora wa Afkica. Hongereni sana wana Simba mnastahili heshima hii, mmeonesha tofauti ya mashabiki wa mpira na wanywa supu za vibudu.

“Sifa hiii ya Ubora tunapaswa kuilinda na kujivunia maana sio kila mtu anaweza bora. Kuilinda sifa hii ya ubora ni pamoja na kuwa wavumilivu pindi timu inapopitia nyakati ngumu,” amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: