Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hii ndio falsafa ya Soka la Benchikha

Abdelhak Benchikha PR Kocha mpya wa Simba, Abdelhak Benchikha

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mpya wa Simba, Abdelhak Benchikha mfumo wake unafanana kidogo na ule aliokuwa anautumia Robertinho akiwa anatumia mfumo wa 4-2-3-1, ambao mara nyingi amekuwa akijilinda na kuepuka timu yake kuruhusu mabao.

Anatajwa kuwa mmoja kati ya wale ambao wanapenda kutwaa makombe makubwa Afrika, lakini huweka nguvu kwenye kombe moja tu kwa msimu mzima kama timu yake inawania makombe mengi kwa kipindi hicho.

Msimu uliopita wakati timu yake ya USM Algier ikitwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho aliwashangaza mashabiki wa timu hiyo baada ya kuachana na ligi ya ndani na kuweka nguvu zake zote kwenye michuano hiyo ya Afrika, lakini mara kwa mara akiwaeleza watafurahi mwishoni.

Katika msimu huu pamoja na Algier kutajwa kuwa kati ya timu bora za Afrika, timu hiyo ilimaliza ligi kuu ikishika nafasi ya 12 kati ya timu 16 kwenye ligi hiyo ya tatu kwa ubora Afrika. Katika michezo 30, timu yake ilipata ushindi kwenye michezo saba tu na kutoka sare 11, huku ikipoteza michezo 12, lakini kwenye shirikisho akatwaa ubingwa mbele ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: