Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Simba yafunguka usajili wa Msuva

Ahmed X Msuva Hatimaye Simba yafunguka usajili wa Msuva

Tue, 22 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Siba imevunja ukimya kuhusu tetesi za kumsajili winga wa Timu ya taifa ya Tanzania, Simon Happygod Msuva ambaye kwa sasa nimchezaji huru.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Simba Sc, Ahmed Ally ambaye ameweka wazi kuhusu tetesi za viongozi wa Simba kuisaka saini ya winga huyo ambaye pia anatajwa kuibukia Yanga ambako alishawahi kucheza kwa mafanikio makubwa miaka ya nyuma.

"Sina hakika sana kuhusiana na hilo lakini na mimi nimekuwa nikiona taarifa mitandaoni, matharani umesema viongozi wangu wameonekana na Msuva basi watakuwa wanajaribu kufanya maamuzi yaliyokuwa sahihi.

"Hakuna timu ambayo isingependa kuwa na Simon Msuva, ni winga wa kisasa, ni mchezaji mzuri, kijana wa nyumbani mwenye uwezo mkubwa na analifahamu soka la hapa Tanzania.

"Kwa hiyo ni ‘potential’ kubwa na ukiwa naye maana yake unajihakikishia kuwa na mtu aliye bora kwelikweli. Yote kwa yote tusubiri taarifa kutoka uongozi wa juu unasemaje," amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: