Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haka ndiko ka mchezo ka viongozi wa Simba

Djuma Shabani WA0027 Haka ndiko ka mchezo ka viongozi wa Simba

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Habari zinazagaa Sasa kumbe Simba walikuwa wa Kwanza kuisaka huduma ya Beki Shaban Djuma wakati akiwa AS Vita, lakini waliamini mazungumzo ya Simu kuliko kwenda kumaliza Dili uso kwa uso.

Injinia Hersi Said alisafiri kwenda Kongo na akamalizana na Shaban Djuma. Matajiri wa Simba kusikia jamaa amemalizana na Yanga wakamwambia arudishe Hela. Djuma alikataa kwani hakuona umuhimu kuwafanyia Yanga hivyo.

Hapa Kuna kitu kama wanasoka naomba tujifunze. Wenzetu Ulaya wakihitaji huduma ya Nyota Fulani watatuma watu mara Kwa mara kufuatilia kiwango na mienendo yake ili kujiridhisha kama anafaa.

Lakini mara Kwa mara watakutana Viongozi, Wawakilishi au Meneja wa Mchezaji husika kuona kama wanaweza kufanya jambo likawa rahisi kabisa. Lakini Shaban Djuma anasema Viongozi wa Simba walitumia Simu kuwasiliana nae, twende tararibu.

Hapo kati Kuna wachezaji kadhaa ambao walijiunnga na Yanga huku mwanzoni wakitajwa kujiunga na Simba. Lakini Yanga walifanikiwa mbele ya Simba ambao wamejijengea Brand yao kiasi cha kuwavutia wachezaji kadhaa.

Mnaikumbuka ishu ya Stephanie Aziz Ki? mabosi wa Simba waliitaka huduma ya Jamaa lakini wakataka kutumia njia rahisi. Unajua nini kilitokea? Eng Hersi Said alikwenda Moja Kwa moja na kumalizana na Aziz Ki.

Sasa tunaweza kusema Simba hawana umafia tena kwenye usajili. Viongozi wa Simba ni kama hawajui kama usajili ni vita ya kujenga Timu Bora Kwa ajili ya Timu yao inayopendwa na Mashabiki wao.

Bila shaka kama Simba wataendelea kupiga Simu, basi wataishia kuona wachezaji wazuri wanacheza Timu jirani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: