Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Ugando aomba radhi tukio la kumkanyaga Henock Inonga

Inonga Ugando Acebook Haji Ugando aomba radhi tukio la kumkanyaga Henock Inonga

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Coastal Union Haji Ugando amemuomba msamaha beki wa Simba Henock Inonga kwa rafu aliyomchezea iliyopelekea beki huyo kuumia mpaka kushindwa kuendelea na mchezo na kuwahishwa Hospitali.

Ugando amesema hakudhamiria kumchezea vibaya kwani yeye si muumini wa vitendo hivyo

“Binafsi imeniumiza sana, na nimesikitika. Sijawahi kufanya kitendo kile kabla.

"Ninamuomba radhi mchezaji mwenzangu, mwanafamilia mwenzangu (Inonga). Sikudhamiria, mimi si muumini wa kufanyiana vitendo vibaya. Mimi ni muumini wa watu kufanyiana Fair,” Haji Ugando amezungumza baada ya mchezo ulioisha kwa timu yake kupoteza kwa goli 3-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: