Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Geoff Leah: Mo Dewji anaiendesha Simba kizamani

Geof Leah X Mo Dewji Geoff Leah: Mo Dewji anaendesha Simba kizamani

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa heshima wa Simba SC Mohamed Dewji jana alitangaza kuteua wajumbe wa bodi ya Baraza la Ushauri la klabu hiyo.

Kufuatia uteuzi huo, mchambuzi wa soka Geoff Lea amehoji Wajumbe hao wanaenda kushauri kitu gani.

"Mimi bado nina wasiwasi, kwangu ninaweza kusema mpira wetu bado kuna vitu vinaendeshwa kizamani. Shida yangu ipo kwenye mambo mawili, jambo la kwanza hawa walioteuliwa wanaenda kushauri kwenye ngwe gani."

"Taarifa inasema wanaenda kushauri bodi lakini hiyo taarifa bado haieleweki wanaenda kufanya majukumu ya kushauri bodi kwa jambo gani na gani."

"Inawezekana hili limefanyika ili kuwaridhisha wale ambao labda walikuwa na kinyongo cha kutengwa. Watu karibu wote walioteuliwa kushika nafasi hizi walishawai kuwa ndani ya klabu, swali la kuuliza, kwanini wameletwa muda huu? kwanini hapo kabla hawakuwepo lakini wameletwa kipindi hiki?"

"Ingewekwa wazi huyu anaenda kutimiza majukumu ya kushauri bodi kwa nafasi hii na hii ingekuwa sawa lakini hii ya kuteuliwa tu kama washauri ni kama wamewekwa tu. Hilo ndilo jambo kubwa linalonipa mashaka."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: