Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gamondi aibuka Kwa Mkapa kuisoma Simba

Gamondi Kwa Mkapa Gamondi aibuka Kwa Mkapa kuisoma Simba

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi na Meneja wa timu hiyo Walter Haryson wametinga katika Uwanja wa Mkapa kutazama mchezo wa Ligi kuu Bara kati ya Simba dhidi ya Ihefu.

Gamondi ameingia mapema kwenye uwanja nusu saa kabla ya mchezo huo kuanza na kushuhudia wachezaji wa timu hizo wakipasha misuli joto.

Gamondi amefika uwanjani kwa ajili ya kuwatazama wapinzani wao Simba ambao watakutana mchezo unaofuata Novemba 5 mwaka huu katika uwanja huo huo.

Kocha huyo amekuwa na utaratibu wa kwenda kutazama mechi wapinzani wao Simba kwani hata kwenye mchezo wa African Football League dhidi ya Al Ahly alikuwepo uwanjani.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: