Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fred Michael asipewe 'thank you'

Fredy WA0007 Fred Michael asipewe 'thank you'

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji Freddy Kouablan ni kama amejitafuta na sasa anaelekea kujipata, licha ya kutokubalika na baadhi ya Mashabiki wa Simba tayari ameweka mabao sita nyavuni kwenye Ligi Kuu msimu huu licha ya kusajiliwa kipindi cha dirisha dogo la usajili.

Kwa washambuliaji asilia yaani namba 9 wanaocheza kwasasa kwenye Ligi Kuu, Freddy amezidiwa mabao na Waziri Junior wa KMC mwenye mabao 12, Samson Mbagula wa Tanzania Prisons mwenye mabao 08 na Adam Adam wa Mashujaa mwenye mabao 07.

Wengine waliomzidi ni viungo kutoka timu mbalimbali wanaocheza Ligi kuu kwa sasa. Hata hivyo Freddy amebakiza mabao 02 kumfikia mtangulizi wake Jean Baleke aliyefunga mabao 08 kabla ya kutimkia nchini Libya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: