Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Football Economy: Mishahara ya Simba inalipa Wachezaji wawili tu Ahly

Simba Vs Ahly Vikosi Football Economy: Mishahara ya Simba inalipa Wachezaji wawili tu Ahly

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba ikionekana kukwamba kwa mara nyingine mbele ya vigogo Al Ahly na kutupwa nje hatua ya Robo Fainali ya Michuano mipya yenye utajiri mkubwa ya African Football League.

Mtaalamu wa masuala ya Chapa, Biko Scanda amefafanua kiuchumi kwa nini Simba imeshindwa kuruka kiunzi mbele ya Ahly.

Akizungumza Biko anasema

"Walikuwa wanashindana timu mbili toka dunia tofauti, ni kama vile treni ya umeme na hii ambayo tumeizoea inafuka moshi. Al Ahly imewekeza kiasi kikubwa cha fedha katika uendeshaji barani Afrika na kuifanya iwe klabu ya karne"

"Simba kwa bajeti yao ya mwaka wa fedha 2023/24 ni bilioni 23 na inalipa mishahara kwenye milioni 500 mpaka 600 ambazo ni kama bilioni 7 kwa msimu mzima, Al Ahly inafanya hivyo kwa wachezaji wawili tu, ni jambo la kuwapongeza wachezaji Simba kwa kuvuja jasho kwa kiasi cha kuonekana wako kiwango sawa na Al Ahly"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: