Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Figisu! Simba yabadilishiwa uwanja Botswana

Simba Mtihani Mzito Dhidi Ya Jwaneng Galaxy Wikiendi Hii.jpeg Figisu! Simba yabadilishiwa uwanja Botswana

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezo kati ya Jwaneng Galaxy na Simba wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya pili ambao awali ulipangwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Botswana, sasa utachezwa kwenye Uwanja wa Obed Itani Chilume mjini Francistown ambao ni kilometa 400 kutoka mji mkuu wa Gaborone.

Mechi hiyo itapigwa Jumamosi Desemba 2 saa 10 jioni, Simba itakuwa ikisaka pointi tatu baada ya kuanza na sare nyumbani huku Jwaneng ikiingia na morali baada ya kuchukua pointi tatu ugenini kwa Wydad Casablanca.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetaja sababu ya kufungia uwanja huo ni kutokidhi vigezo huku kikosi cha Simba kikitarajiwa kusafiri Ijumaa.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amethibitisha taarifa hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: