Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fahamu mtonyo watakaopiga Simba Sc Super League

Simba SC Kwa PD Fahamu mtonyo watakaopiga Simba Sc Super League

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pesa iliyowekwa kwa ajili ya michuano hiyo kwa vilabu ni kiasi cha dola za Kimarekani milioni 10.3 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 25 za Kitanzania.

Pesa zote zinatolewa na Kampuni inayojihusisha na Michezo ya Kiitaliano ambayo ndio watadhamini michuano hiyo (Mpaka sasa haijawekwa wazi) ila Makao Makuu yake yapo Kigali Rwanda.

Mashindano yana timu nane ambazo ni; Simba Sports ???? Al Ahly TP Mazembe ???? Esperance Enyimba ???? Wydad Casablanca Petro Luanda ???? Mamelodi Sundowns

1. Kila timu inayoshiriki itapokea kiasi cha dola za Kimarekani 700,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 1.76 za Kitanzania.

2. Timu itakayofuzu hatua ya Nusu Fainali inatarajia kupewa kiasi cha Dola 800,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 2.01 za Kitanzania, hivyo ukijumuisha na ile ya kupewa kwa kushiriki tu (dola 700,000) jumla itachukuwa shilingi Bilioni 3.75 za Kitanzania.

3. Timu itakayoshika nafasi ya pili (Bingwa mtetezi wa #AfricanFootballLeague) atapewa kiasi cha Dola za Kimarekani 500,000 ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 1.26 za Kitanzania na ukijumuisha na zile alizopewa baada ya kufanikiwa kufika nusu fainali (800,000) na zile wanazopewa kila timu (700,000) jumla anakuwa amepata dola Milioni mbili ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 5.03 za Kitanzania.

4. Bingwa wa Mashindano haya ya #AfricanFootballLeague atapewa zawadi cha Dollar za Kimarekani Milioni moja ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 2.52 za Kitanzania na ukijumuisha na zile alizopewa kwa kushiriki mashindano pamoja na kufuzu hatua ya Nusu Fainali hivyo Bingwa atapata jumla ya dollar za Kimarekani Milioni mbili na nusu ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 6.29 za Kitanzania.

FIFA wameweka kiasi hicho cha pesa kwa vilabu ili zawadi zisizidi kiasi kile ambacho hupata timu zinazoshiriki Mashindano ya Klabu Bingwa ya Dunia ambapo Bingwa hupata jumla ya dollar za Kimarekani Milioni tano na Bingwa mtetezi hupata kiasi cha Dollar za Kimarekani Milioni mbili na nusu.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuzinduliwa katika Dimba la Mkapa mnamo Oktoba 20, 2023 kati ya Simba na Al Ahly na yatatamatika kwenye mechi ya Fainali Novemba 11, 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: