Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fabrice Ngoma kutambulishwa leo Simba?

Fabrice Ngoma Tt Fabrice Ngoma kutambulishwa leo Simba?

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba huwenda wakamtambulisha, Fabrice Luamba Ngoma aliyekuwa akihusishwa na timu hiyo kwenye kipindi hiki cha usajili.

Fabrice Ngoma anayecheza nafasi ya Kiungo ni mchezaji anayedaiwa kuwa ‘Umafia’ mkubwa ulifanyika AirPort usiku wa manane kwa kupitishwa mlango wa uwani na kujikuta Unyamani huku majirani wakiachwa hawaamini macho yao.

N0. 6 hiyo ya mpira raia wa Congo mwenye umri wa miaka 29 inadaiwa alifika Julius Nyerere International Airport kupitia Ndege ya Ethiopian Airline usiku huo lakini ‘Makomando’ wa Lunyasi wakafanya kazi yao na kuwaacha baadhi ya Uongozi wa Majirani waliyojitokeza kwa shangwe na bashasha wapigwe na Baridi huku wasijue chakufanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: