Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edo Kumwembe: Nafasi ni ngumu kwa Simba kwenda Robo Fainali

Simba Na Benchikha Wote Wana Tabia Sawa   Edo Edo Kumwembe: Nafasi ni ngumu kwa Simba kwenda Robo Fainali

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba ikijiandaa kupambana na Wydad ugenini mchezo wa tatu wa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchambuzi wa Michezo kutoka Wasafi FM, Edo Kumwembe anasema kuna ugumu sana kwa Simba kuweza kuvuka hatua ya Makundi.

Akizungumza Edpo anasema;

“Nafasi ya Simba kwenda robo Fainali imeanza kuwa ngumu zaidi. Simba wameambulia pointi mbili katika mechi zao mbili za mwanzo. Na sasa wana safari ya kukabiliana na Wydad pale Morocco. Mechi mbili zijazo watacheza na hawa jamaa wa Afrika Kaskazini wakianzia na pambano la ugenini ambalo litakuwa la machozi jasho na damu kwa wenyeji".

"Tayari Wydad wamepoteza mechi mbili. Moja nyumbani dhidi ya Jwaneng nyingine wamepoteza juzi Jumamosi dhidi ya ASEC Mimosas. Pambano hili dhidi ya Simba watalitumia kwa kujaribu kuwafuta machozi mashabiki wao. Hawatataka kufungwa mechi ya pili mfululizo nyumbani, au mechi ya tatu mfululizo katika kundi. Simba wana kazi. Kama Simba wataweza kufanya vema katika mechi mbili zijazo dhidi ya Wydad, huku ASEC na Jwaneng wakipunguzana wenyewe kwa wenyewe inaweza kuwasaidia. Tatizo ni kwa Simba ipi? Hii ya Onana? Benchikha ana kazi kubwa ya kufanya. Tusubiri tuone.”

Je unamuona mnyama akienda hatua inayofuata? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: