Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coastal Union walitaka wenyewe kufungwa vile na Simba - Mchambuzi

Simbasctanzania 1695308311566.jpeg Coastal Union walitaka wenyewe kufungwa vile na Simba - Mchambuzi

Fri, 22 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia East Africa Radio, Abissay Stephen amesema kuwa Klabu ya Soka ya Coastal Union ya Tanga walitaka wao wenyewe kufungwa mabao 3-0 na Simba Sc katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC jana pale Uhuru Stadium.

Mabao yote ya Simba yalifungwa na mchambuliaji wao, Jean Baleke raia wa Congo DR dakika ya 6, dakika ya 12 na dakika ta 40 kwa mkwaju wa penati.

"Niliona mabao ambayo Simba amefunga ndani ya dakika zile ni mabao ambayo Coastal Union unaweza ukasema yeye ni kana kwamba alitaka afungwe vile.

"Wakati naangalia game nilikuwa nasema kuwa hizi dakika za mapema zinatuonesha kweli kwamba jana (juzi) Namungo alifanya kazi dhidi ya Yanga, kwa sababu alijua nakutana na timu ambayo ni free scoring team kwenye ligi.

"Kwa hiyo mimi Namungo FC nisipokuwa na nidhamu dakika 10 naweza nikapigwa hata bao 2, kwa sababu kuna watu tayari walishapigwa hadi bao 5," amesema Abissay Stephen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: