Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Clatous Chama, ni wakati sahihi wa kuwa Shetani au Malaika

Chama Goal Vs JKT Clatous Chama, ni wakati sahihi wa kuwa Shetani au Malaika

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama nyasi zingekuwa na hisia zisingechoka kueleza ubora wa miguu ya Clatous Chama, pasi na shaka mpira ungekubali ndoa ya milele na miguu mitakatifu kwenye ardhi ya Albert Chalamila.

Kushuhudia miguu ya Clatous Chama ikiwa inasogelea mpira ni maonyesho bora kwenye mboni ya macho yangu. Ni zaidi ya ile burudani ya kumshuhudia Hamisa mobetto akiwa kitandani na khanga moja.

Wakati huu dunia ikizidisha hila juu ya wachezaji waliotunukiwa kipaji halisi cha kucheza namba 10 kwa hoja dhaifu eti hawawezi kupress. Ardhi yetu imepati bahati ya kutunikiwa, Clatous Chama.

Ni burudani ilioje kuitazama miguu ya Clatous Chama ikitenda miujiza, taarifa mbaya inayopenya kwenye masikio na kuhuzunia ubongo kwa wana simba muda huu ni je Clatous Chama atabaki msimbazi?

Mwanzo aliamua kuwa shetani na kuwaacha mashabiki wekundu wakibaki na vilio vya kusaga meno, ni wakati huo mashujaa wao wawili walipochagua kuwa mashetani na kuondoka zao. Clatous Chama alienda zake Rs Berkane huku Jose Miquisson akienda kwa mafarao.

Kama Clatous Chama atachagua kuwa malaika jina lake litapigwa mihuri ya moto kwenye paji la uso la kila shabiki wa simba milele, kama akiamua kuwa shetani na kuondoka zake ni wazi mioyo ya mashabiki haitochoka kulikumbuka jina lake.

Akiondoka vilio zitatawala, huzuni hazitoweza kufukuzwa na furaha, wapo watakao busu jezi yake kwa wema. Wapo watakaolichoma jezi yake kwa hasira ni wazi baadhi watashindwa kuzuia hasira zilizoambatana na mfadhaiko.

Akibaki utakuwa muendelezo usio na kikomo wa utawala wake. Miguu yake itaendelea kusujudiwa kwa miujiza yake. Wapo watakao sahau nidhamu yake inayosemeka kuwa na udhaifu.

Clatous Chama ni wakati sahihi sasa wa kuwa shetani au malaika

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: