Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Clatous Chama hakustahili kubeba tuzo yoyote msimu huu?

Chama Best Goal Clatous Chama

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Simba SC, Clatous Chota Chama hakufanikiwa kubeba Tuzo yoyote katika Tuzo zilizotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF Juni 12.

Chama alibahatika kuingia katika kikosi bora cha msimu huku Saido na Mayele wakitawala tuzo hizo kwa siku ya jana.

Namba za Chama msimu huu sio za kitoto jambo linalotia wasiwasi kuamini kuwa hakustahili kunyakua Tuzo yoyote.

Clatous Chama kwenye Nbc Premier League msimu huu uliomalizika.

Mechi 22 Mechi alizoanza 22 Mabao 4 Pasi za mabao 14 Amehusika katika mabao 18 Dakika kwa kila kuhusika kwa bao 106

Ndiye mchezaji aliyemaliza na pasi nyingi za mabao kwenye msimu wa Nbc Premier League 2022-23.

Ndiye mchezaji watatu kuhusika katika mabao mengi kwenye msimu wa Nbc Premier League 2022-23.

Ndiye mchezaji pekee aliyeweza kutoa angalau pasi mbili za mabao kwenye mechi nyingi tofauti za Nbc Premier League 2022-23, amefanya hivyo katika mechi tano tofauti.

Sasa amemaliza na angalau pasi za mabao 14 ndani msimu mmoja wa Nbc Premier League kwa mara ya pili katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita.

2020-21 (pasi za mabao 15) 2022-23 (pasi za mabao 14)

Je ni kweli hakustahili tuzo yoyote? Tuachie maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: