Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama kimataifa ni habari nyingine CAF

Chama Hat Trick Chama

Fri, 7 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Clatous Chama, raia wa Zambia nyota wa Simba kwenye anga la kimataifa ni habari nyingine kutokana na kuhusika kwenye mabao mengi ya kufunga katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi wakiwa na pointi 9 kundi C.

Simba ikiwa imefunga mabao 10 baada ya kucheza mechi sita kahusika kwenye mabao matano huku akiwa amesepa na mpira mmoja baada ya kufunga hat trick moja.

Ni mabao manne kafunga, kawatungua Vipers bao moja na Horoya mabao manne na kwenye mchezo huo alitoa pasi moja waliposhinda mabao 7-0 ukiwa ni ushindi mkubwa kwa Simba kwenye hatua ya makundi msimu huu.

Mbali na kusepa na mpira pia ana tuzo ya kuwa mchezaji bora mechi ya nne na alipenya kwenye kikosi cha kwanza mechi ya nne pamoja na ile ya tano pamoja na bao lake dhidi ya Horoya ambalo lilikuwa ni pigo la faulo kuchaguliwa kuwa bao bora.

Kwa upande wa Yanga mkali wao ni Fiston Mayele mwenye mabao matatu katika hatua ya makundi Kombe la Shirikisho na ana tuzo ya bao bora dhidi ya US Monastir.

Mayele anashikilia rekodi ya kuwatungua nje ndani Real Bamako bao mojamoja kwenye mechi mbili mfululizo ni chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.

Imetupia mabao 9 kwenye hatua ya makundi huku Mayele akihusika kwenye mabao manne, kafunga matatu na ana pasi moja ya bao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: