Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama bado ni Mfalme kwa Benchikha

Chama X Benchikhaaaa Chama bado ni Mfalme kwa Benchikha

Tue, 5 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji mmoja wa kigeni wa Azam FC aliposikia Abdelhak Benchikha amekbidhiwa mikoba ya kuinoa Simba akasema mchezaji wa kwanza kuondoka Msimbazi atakuwa Clatous Chota Chama.

Nyota huyo wa Wana Lambalamba alisema hivyo kutokana na maisha ya kifalme aliyokuwa akiishi Chama ndani ya kikosi cha Simba.

Baada ya Benchikha kutua kweli kulikuwa na kila dalili kwamba Mwamba wa Lusaka ataondoka Simba na kuhitimisha ufalme wake klabuni hapo.

MVIVU WA MAZOEZI, MCHOCHEZI Kocha Benchika ilionekana kama vile alipewa faili la Chama, akaanza kutoa msimamo wake kuhusu wachezaji wa Simba. Benchika akasema kwake hakuna staa mkubwa zaidi ya timu. Kila mchezaji akatakiwa kuwa na nidhamu na kujituma kwa ajili ya timu.

Mtego huo ukamnasa Chama baada ya kuonekana mvivu, sio mpambanaji na kuanza kutolewa katika michezo kadhaa. Haikuwa ajabu nyota huyo raia wa Zambia kuanzia benchi.

Pia, Chama akanasa kwenye mtego mwengine wa utovu wa nidhamu katika mchezo dhidi ya Wydad jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa kwamba nyota huyo alitupiana maneno na mmoja kati ya wasaidizi wa Benchikha.

NJIA NYEUPE KUONDOKA SIMBA Katika kipindi hiki njia ya Chama kuondoka Simba ilishaandaliwa. Kila Mwana Simba alikubali Chama aondoke Simba.

Maneno mengi yalizungumzwa juu yake huku wengine wakikumbusha tabia yake ya kuigomea timu hususan alipokataa kwenda kambini Uturuki mwanzoni mwa msimu. Kila Mwanasimba ni kama alichoshwa na vitendo vya utovu wa nidhamu.

AIGAWANYA TIMU Chama akasimamiswa hata hivyo, alipopelekwa katika Kamati ya nidhamu ya Simba , wanakati Chini ya Mwenyekiti, Suleiman Kova, wajumbe waligawanyika pande mbili. Wengine wakisema aachwe kwenye dirisha dogo na wangine wakipinga.

Bahati nzuri michuano yote ilikuwa imesimama kutokana na Afcon. Chama aliporudi baada ya mashindano hayo katika mazingira ya kutatanisha Klabu ya Simba ikatangaza kumsamehe huku tetesi zikidai ataachwa mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wake utaisha.

AGEUKA LULU KANDA YA ZIWA Dhidi ya Mashujaa, Chama aliupiga mwingi, dhidi ya Tabora United akafunika, akakipiga sana dhidi ya Azam FC na Geita Gold. Pia, alicheza vizuri dhidi ya Asec Mimosa ugenini.

Baada ya mechi za Ligi Kuu za Kanda ya Ziwa, mawazo ya mashabiki na wanachama wa Simba yakabadilika. Kila mmoja wao akataka Chama apewe mkataba mpya.

FUNGAKAZI NA JWANENGY GALLAX Katika mchezo huo wa kuhutisha hatua ya makurdi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Chama alibeba Simba mabegani mwake. Kwa kila mmoja ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo.

Chama alitoa assisti mbili na kuanzisha mwendo wa mabao mengine. Aliupiga mwingi sana. Alikuwa Chama wa tofauti sana, alizaliwa upya na kuonesha ufundi wake ambao mashabiki wa Simba hawajauona kwa siku nyingi.

Chama alishindania mipira, alikimbia na kuiwahi mipira mirefu iliyopigwa na wachezaji wenzake na hata aliyojitangulizia mwenyewe. Hakuwa Chama yule mvivu tena, alikuwa mpambanaji hasa.

KALI YA YOTE Mara baada ya kufunga bao lake (la nne) alikimbia na kwenda kumkumbatia Benchikha! Kocha yuleyule aliyedhaniwa kwamba angeweza kuhitimisha safari ya ufalme wake Msimbazi.

Ni dhahiri Benchikha sasa anamkubali Chama, anaujubali ufalme wake na anamoanga kikosi cha kwanza.

Je, kasi hii na uwezo huu wa Chama ni kutokana kubakiza miezi mitatu katika mkataba wake au ni mabadiliko ya kudumu?

Huku mitaani mashabiki wa Simba wants email Chama apewe mkataba mpya haraka iwezekanavyo. Tena wanasisitiza, sio mkataba mpya tu, bali mkataba mnono.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: