Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama aondoke, ni mbovu - Shabiki Simba

Pacome Chama Pc Chama aondoke, ni mbovu - Shabiki Simba

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Simba SC, Mchome Mapovu amesema kuwa kiungo wao mshambuliaji, Clatous Chama ameshuka kiwango hivyo anapaswa kuachwa na timu hiyo ama kutafutiwa mbadala wake.

Mchome amesema hayo baada ya Simba kukubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons juzi katika uwanja wa CCM Jamhuri mjini Morogoro.

“Chama ni mchezaji mwenye historia kubwa sana Tanzania, ukitafuta wachezaji wenye record nzuri kwa misimu takribani mitano nyuma kwa Tanzania, Chama yumo lakini kwa sasa ni mchezaji wa mechi moja moja, mpaka aone kuna kaudhaifu flani kwenye timu utamuona ni bonge la mchezaji.

“Chama huyu ni mbovu vibaya mno, akikutana na mabeki wanaofika miguuni, hawezi kuibeba timu. Ndiyo maana nasema mjadala wa Pacome na Chama tuuache. Pacome yupo juu lakini Chama alikuwa amebuma, amekuja kuonekana kwenye mechi ya Jwaneng Galaxy tu, ni aina ya mchezaji anaibuka kwenye mechi moja anazima.

“Pacome ana mwendelezo kwenye ligi na hata kimataifa lakini Chama haonekani mpaka umtafute uwanjani. Chama amepotea, anacheza haeleweki. Chama tumchukulie kama mchezaji wa kimataifa.

“Chama abaki kwa sababu kwenye hizo mechi moja moja anzoamua anatusaidia kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine lakini atafutiwe mbadala wake lakini kama uwepo wake unakwamisha wachezaji wengine kusajiliwa basi aachwe. Kuna wake akiwa kwenye siku zake vizuri anatusaidia,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: