Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama anaweza kucheza bila kuelekezwa na Benchikha - Ahmed Ally

Chama Vs Jwaneng.jpeg Clatous Chota Chama.

Fri, 8 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema kuwa hakuna ugumu wowote wa kucheza mchezo bila kuwa na kocha wao mkuu, Abdelhak Benchikha.

Ahmed amesema hayo mara baada ya kutua Tanga kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Coastal Union utakaopigwa kesho Jumamosi katika Dimba la Mkwakwani huku Mnyama akiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Tanzania Prisons kwa kipigo cha bao 2-1.

Benchika ameondoka jana Simba kuelekea nchini kwao Algeria kwa ajili ya kuhudhuria kozi fupi ya siku tano huku akiiacha timu chini ya kocha msaidizi Farid Zemiti.

"Chama (Clatous) anaweza akacheza bila hata kufundishwa na kocha. Chama ameumbwa kucheza mpira, miongoni mwa kazi ambazo alipewa Chama ukiachana na kuishi, basi ni kucheza mpira. Mtu kama Chama unakuwa na mashaka kwamba atashindwa kucheza kwa sababu kocha hayupo?

"Niwatoe hofu mashabiki wa Simba, timu itacheza kwa ubora uleule hata kama mwalimu hayupo kwa sababu wachezaji wanaelewa falsafa, maelekezo na mahitaji ya mwalimu. Tunao wachezaji ambao ni wakomavu ambao wana uwezo wa kufanya chochote wakati wowote.

"Benchikha atakuwa nyumbani kwao Algeria kimwili lakini atakuwa uwanjani kifalsafa," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: