Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama ampa mzigo mzito Luis Miquissone

Chama X Miquissone Mtibwa Chama ampa mzigo mzito Luis Miquissone

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Simba, Mzambia Clatous Chama, amemtaka kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Luis Miquissone, ahakikishe anampa pasi za mwisho 10 kwa ajili ya kufunga mabao katika msimu huu mpya ulioanza Agosti 15, mwaka huu.

Chama ametoa kauli hiyo kufuatia Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wake wa juzi uliochezwa kwenye Uwanja wa Manungu Complex ulioko Turiani, Morogoro.

Katika ushindi wa mchezo huo, Chama alifunga bao la nne baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Miquissone ambaye amerejea tena katika timu hiyo akitokea Al Ahly ya Misri.

Chama alisema anaimani kubwa atafanya vyema na vizuri msimu huu kwa kufunga mabao kutokana na muunganyiko mzuri wa wachezaji wenzake hasa Miquissone ambaye aliwahi kucheza naye miaka ya nyuma.

Chama alisema anafurahi Simba kupata ushindi wa mabao 4-2, huku yeye pia akifunga katika ushindi huo wa kwanza msimu huu.

“Nimefurahi kupata pasi ya mwisho na kufunga kutoka kwa Miquissone (Luis), ila nataka assist 10 kutoka kwa nyota huyo katika michezo iliyopo mbele yetu,” alisema kiungo huyo.

Aliongeza kwa ubora wa kikosi chao, anaimani wanatarajia watafanya vizuri zaidi ya msimu uliopita na hiyo inatokana na maboresho yaliyofanyika kwa kusajili wachezaji wapya ambao wamekuja kusaidia kufikia malengo ya kutwaa mataji mbalimbali yaliyopo mbele yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: