Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chama: Hakuna haja ya kunyoosheana vidole, tushikamane pamoja

Chama Atoa Kauli Nzito Kuelekea Mchezo Dhidi Ya Power Dynamos.jpeg Kiungo wa Simba, Clatous Chama

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Simba SC, Clatous Chota Chama ameomba kuungana katika nyakati hizi ambazo kumekuwa na minong’ono ya hapa na pale tangu kumalizika kwa #DerbyYaKariakoo Novemba 5. 2023.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chama ameandika “Katika nyakati hizi hakuna haja ya kunyoosheana vidole na kutupiana lawama, haitotusaidia kwa namna yoyote ile. Huu ni wakati sahihi wa kushikamana pamoja na kuunganisha nyoyo zetu. Twendeni tena leo tukiwa na nguvu moja na kufanya kazi ili kurejea katika ari yetu”

Mnyama leo atashuka dimbani kuvaana na Namungo FC katika muendelezo wa mikikimikiki ya NBC Premier League.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: