Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#CAFUPDATES: Half Time' Simba 2-0 Wyda, Onana wa moto balaa

Onana Goal Vs Wydad.jpeg #CAFUPDATES: Half Time' Simba 2-0 Wyda, Onana wa moto balaa

Tue, 19 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kumaliza kipindi cha kwanza cha ikiwa inaongoza kwa mabao 2-0, dhidi ya Wydad Casablanca, Simba imefanikiwa kuweka rekodi tofauti tofauti.

Kwanza ndio imekuwa timu pekee kutoka Tanzania kumaliza kipindi cha kwanza cha mchezo wa Ligi ya Mabingwa ikiwa inaon-goza msimu huu kwenye hatua ya makundi.

Vilevile imekuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kwenye michuano ya msimu huu kufunga mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo wa hatua ya makundi.

Pia kiungo mshambuliaji Andre Onana ameweka rekodi ya kuwa mchezaji pekee kutoka timu ya Tanzania katika michuano ya msimu huu kufunga mabao mawili kwenye kipindi cha kwanza.

Timu nyingine inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kutoka Tanzania ni Yanga, ambayo itacheza kesho na Medeama saa 10:00 kwenye Uwanja wa Mkapa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: