Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF walitaka timu bora, Simba tujidai - Ahmed Ally

Image 115 Ahmed Ally.png CAF walitaka timu bora, Simba tujidai - Ahmed Ally

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahemd Ally amesema kuwa mashabiki wa klabu hiyo wanatakiwa kutembea vifua mbele kwani timu yao ni miongoni mwa timu Bora Barani Afrika ndiyo maana imekuwa miongoni mwa timu 8 pekee Afrika nzima ambazo zitashiriki mashindano ya African Football League.

Ahmed amesema hayo kuelekea mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo utakaofanyika Ijumaa ijayo Oktoba 20, 2023 katika Dimba la Mkapa kati ya Simba SC na Al Ahly ya Misri.

"Lazima tujidai kweli kweli, lazima tujizunie. Wakati sisi tunaangaika na timu namba moja Afrika wengine eti wanajidai na Dar Derby. Tunahangaika kumleta Infantino, Motsepe na viongozi wengine wakubwa. Tuna haki ya kujidai sana.

"Tumefanya kazi kubwa sana hadi kupata hii nafasi, kwa mtu wa kawaida anaweza kudhani CAF walitaka timu kila nchi lakini ukweli wao walitaka timu bora kutoka kila ukanda.

"Yani CAF wakianzisha mashindano ya timu nne sisi tutakuwepo. Wengine kupata nafasi lazima mashindano yawe na timu 20 kwenda mbele," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: