Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bocco: Yaliyopita si muhimu tena, tunatizama mbele

John Bocco AFL Nahodha wa Simba, John Bocco

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa klabu ya Simba Sc John Raphael Bocco akielezea maandalizi na mipango yao kuelekea mchezo wa leo dhidi ya Namungo FC amesema kupoteza mbele ya Yanga ni sehemu ya mchezo na hiyo haiwatoi katika malengo waliyojipangia msimu huu.

Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari Bocco amesema;

"Wachezaji wote maandalizi yetu ni mazuri kwenye huu mchezo kuhakikisha tunapata alama tatu. Tumejiandaa Kulingana na aina ya mpinzani ambaye tutakutana nae ili kupata ushindi. Hatuangalii kilichopita tunaenda kukutana na mpinzani mgumu ila tutapambana na kupata matokeo mazuri dhidi yao."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: