Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha hakuwa kocha sahihi kwa Simba - Mchambuzi

BENCHIKHA Age 2024 04 29 At 22.jpeg Benchikha hakuwa kocha sahihi kwa Simba - Mchambuzi

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka kituo cha runinga cha TV3, Boiboi Mkali amedai kuwa aliyekuwa Kocha wa Simba SC, Abdelhak Benchikha hakuwa kocha sahihi kwa timu hiyo.

Boiboi amesema hayo baada ya kocha huyo aliyejiunga na Simba mwishoni mwa mwaka jana (2023) kubwaga manyanga na kuipiga chini timu hiyo akivunja mkataba yeye na wasaidizi wake wawili na kurudi nyumbani kwao Algeria.

"Wakati Benchikha anakuja Simba tulisema sisi kuwa huyu sio kocha sahihi kuifundisha Simba lakini tulitukanwa sana na tulionekana sisi hatujui kitu.

"Benchikha hakupaswa kuja Simba, huyu sio kocha wakuifundusha Simba kwa sababu yeye ni kocha wa mataji na sio kuijenga timu.

"Simba walikuwa wanahitaji kocha wakuijenga timu kwa sababu wakati anakuja Benchikah timu ilikuwa tayari imeshavurugika hivyo walihitaji kocha ambayee ataijenga timu.

"Tatizo sisi tukiongea tunaonekana hatujui kitu lakini huwa tunaonaga mbali kwa sababu tunazijua timu zetu," amesema Boiboi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: