Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha ateua 22 wa kuiua ASEC Ligi ya Mabingwa

IMG 8911.jpeg Benchikha ateua 22 wa kuiua ASEC Ligi ya Mabingwa

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mualgeria, Abdelhak Benchika ameteua wachezaji 22 kwa safari ya Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wa Kundi B Ligi ya Mbingwa Afrika dhidi ya wenyeji, ASEC Mimosas Ijumaa.

Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny Jijini Abidjan utaanza Saa 4:00 usiku kwa Saa za Tanzania.

Kuelekea mechi mbili za mwisho, Simba SC inashika nafasi ya pili Kundi B ikiwa na pointi tano, nyuma ya ASEC Mimosas yenye pointi 10 na mbele ya Jwaneng Galaxy ya Botswana yenye pointi nne na Wydad Athletic ya Morocco yenye pointi tatu baada ya wote kucheza mechi nne.

Wakati ASEC wakiwa wenyeji wa Simba wikiendi hii, Wydad watakuwa wageni wa Jwaneng Galaxy huko Botswana.

Mechi za mwisho ni Simba na Jwaneng Galaxy Jijini Dar es Salaam na Wydad dhidi ya ASEC Jijini Casablanca.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: