Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha apewe maua yake

Benchikha Simba Ms Benchikha apewe maua yake

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiukweli kocha Abdelhak Benchika juzi amefanya kazi yake kwa ufanisi wa asilimia 100 hakuna aliyetarajia Simba mbovu kuonesha kiwango kikubwa namna ile dhidi ya wababe Wydad Casablanca.

Kocha ameonesha uwezo wa kikubwa sana kuweza kuwatumia wachezaji wa kawaida kucheza mpira wa kikubwa mno.

Goli walilofungwa Simba lilitokana na uzembe binafsi wa wachezaji kocha hastahili hata chembe ya lawama. Kwangu mimi naona kati ya makocha bora kuwahi kuingia Tanzania huyu ni namba moja, tumpe maua yake aisee.

Ukweli usemwe tu Simba na Yanga safari imeisha hakuna mwenye nafasi kusonga mbele kundi la Yanga wanasonga CR Belouizdad na Al Ahly. Kundi la Simba wanasonga mbele ASEC Mimosas na Wydad huo ndio ukweli japo mchungu

ASEC Mimosas anahitaji kushinda mechi moja tu dhidi ya Jwaneng nyumbani na kufikisha pointi 10 huku Simba ikitakiwa kushinda mechi 3 (dhidi ya wydad, jwaneng na ugenini kwa ASEC) Jwaneng anaweza kupigika kirahisi ila ASEC na Wydad kuwazuia mechi ya mwisho ya kusonga mbele itakuwa mtihani wa kuingia peponi.

Kwenye soka lolote linawezekana ila ukishakosea mipango ukashindwa kupata matokeo muhimu mechi za awali jiandae kufungasha virago hakuna ataekubali kukuruhusu upite kirahisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: