Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha amfyeka Saido Simba

IMG 4294 Saido.jpeg Kiungo wa Simba SC, Saido Ntibazonkiza

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya panga la kocha Abdelhak Benchikha kuwapitia wazawa, panga hilo kwa sasa limehamia kwa nyota wa kigeni waliopo Simba na fasta limeanza na kiungo mshambuliaji, Said Ntibazonkiza 'Saido' ambaye inaelezwa amependekeza kwa viongozi afyekwe na wenzake wengine wawili.

Benchikha amewafyeka Nassor Kapama, Shaaban Idd Chilunda, Jimmyson Mwanuke, Abdallah Khamis na kipa chipukizi, Ahmed Feruzi, lakini kwa sasa wakati dirisha dogo likiwa njiani kufungwa Jumatatu ijayo, inaelezwa kocha huyo amewasilisha ripoti ya kufyeka nyota watatu wa kigeni.

Ipo hivi. Simba kwa sasa inapambana kusaka mshambuliaji mmoja mkali wa kumrahisishia kazi Benchikha kwani haridhishwi na washambuliaji waliopo sasa akiwamo Jean Baleke aliye kinara wa mabao kwa sasa wa timu hiyo katika Ligi Kuu Bara akifunga manane.

Katika kuhakikisha anapata nafasi ya kifaa hicho kipya kinaingia Msimbazi, kocha Benchikha tayari amependekeza kwenye ripoti yake, Simba iachane na mshambuliaji Moses Phiri na winga Aubin Kramo ambaye hajaonyesha kutokana na kusumbuliwa na majeraha tangu asajili mapema msimu huu.

Kama haitoshi, pia ametaka kiungo mshambuliaji, Saido naye atemwe kati ya wachezaji watatu aliyowapendekeza kwenye ripioti hiyo iliyo mezani mwa mabosi wa Simba.

Chanzo cha kuaminika kutoka Simba, kinasema kuwa kwa mujibu wa ripoti ya Benchikha kwa viongozi imethibitisha kocha huyo amerithia kuondoka kwa wachezaji hao watatu wa kigeni, ili kupisha usajili mwingine akiwemo mshambuliaji mmoja baada ya kumalizana na Babacar Sarr.

Kiungo huyo mkabaji kutoka Senegal tayari ameshatambulishwa na kuanza kucheza kwenye mechi za michuano ya Kombe la Mapinduzi 2014 inayofikia tamati leo usiku kwa timu hiyo kuvaana na Mlandege kwenye fainali inayiopigwa Uwanja wa New Amaan Complex, mjini Unguja.

"Ripoti ipo chini ya viongozi wakuu na wanaendelea kuifanyia kazi ila, kocha kapendekeza wachezaji watatu wa kigeni waachwe ili kupisha usajili mwingine na miongoni mwa hao watatu yupo Saido, Phiri na Kramo," kimesema chanzo hicho na kuongeza;

"Licha ya kocha kuvutiwa na nidhamu ya Saido, amekiri mwenyewe hawezi kuwa na msaada kikosini hasa kipindi hiki ambacho timu inataka kufikia mafanikio ya kutinga hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa na kutwaa mataji yote tunayoshiriki."

Chanzo hicho kilisema mazungumzo kwaajili ya kumalizana na wachezaji hao yanaendelea huku akiweka wazi kuwa kwa upande wa Saido mambo hayawezi kuwa magumu kwao kwani tayari mkataba wake unamalizika dirisha hili.

"Phiri kinachomuondoa ni kiburi ana misimamo na sio mtu wa kusikiliza kile anachoambiwa hilo chini ya Benchikha sio rahisi kuvumilika na kwa upande wa Kramo ni kutokana na kutoka kwenye kuuguza majeraha, hivyo hakutakuwa na muda wa kumsubiri ili waweze kurudi kwenye ushindani.

"Baada ya kumalizana na wachezaji hao kutakuwa na ongezeko la mchezaji mmoja tena eneo la ushambuliaji ambaye tayari mambo yamekwenda vizuri atatangazwa muda wowote kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumatatu."

Chanzo hicho kilisema kwa sasa mazungumzo na wachezaji hao yanakwenda vizuri na wanataka kumalizana nao vizuri ili kuondoa migogoro baadae hasa kwa wachezaji wawili ambao bado wana mkataba na timu hiyo.

Saido mkataba wa mwaka mmoja alioingia na Simba umemalizika kwani alisajiliwa dirisha dogo la Desemba 24, mwaka juzi akitokea Geita Gold akipewa mwaka mmoja na ulipoisha aliongezewa mwingine wa muda kama huo ambao unamaliza sasa.

Alipotua Simba aliibuka kinara wa mabao akifunga mabao 17 sawa na aliyokuwa nayo, Fiston Mayele aliyekuwa Yanga kabla ya msimu huu kuuzwa Pyramids ya Misri, pkia aliasisti mabao 12 msimu huo wa 2022-2023 na kwa msimu huu tayari ameifungia timu hiyo mabao manne na kuasisti bao moja.

Kabla ya kutua Geita na baadae kuhamia Simba, Saido aliwahi kung'ara na Yanga aliyoichezea kwa misimu miwili kuanzia mwaka 2020 akitokea Vital'O ya Burundi.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: