Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha achora ramani ya maangamizi

Benchikha Mapinduzi.jpeg Benchikha achora ramani ya maangamizi

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: Dar24

Kocha Mkuu wa Simba SC Abdelhak Benchikha amesema tayari amechora ramani ya kuelekea mchezo wa mwisho wa Kundi B, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy, ambapo moja kwa moja amewataka wachezaji wake kuelekea kambini kuanza maandalizi ya mtanange huo.

Simba SC ambayo mchezo uliopita dhidi ya Asec Mimosas, ilitoka suluhu, sasa inahitaji ushindi wa aina yoyote Jumamosi (Machi 02) itakapoikaribisha Jwaneng Galaxy ya Botswana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.

Akizungumza baada ya kuwasili jijini Dar es salaam, Benchikha amesema hii ni mechi muhimu sana kushinda na kwenda hatua ya Robo Fainali, hivyo lazima wapambane na kutafuta matokeo mazuri uwanja wa nyumbani.

Amesema kubwa kwake ni kufanyia kazi nafasi wanazozipata na kushindwa kuzibadili kuwa mabao, hususan kuelekea mchezo huo muhimu ambao wanahitaji ushindi ili kufuzu Robo Fainali ya michuano hiyo kwa mara nyingine.

Benchikha amesema mechi yao na Asec Mimosas walicheza vizuri sana, lakini walishindwa kutumia nafasi iliyopatikana kupitia kwa Sadio Kanoute, ambayo ingekuwa muhimu sana kwao.

“Tunasahau hilo, tumerejea nyumbani kusahihisha makosa yetu, kundi ni gumu sana, lakini kwetu tunataka kushinda mechi yetu ya Jwaneng Galaxy kwa sababu itatuwezesha kufuzu kucheza Robo Fainali kwa mara nyingine.

Tunajua historia ya wapinzani wetu miaka ya nyuma, lakini haihitaji kuiweka akili zaidi ya kuandaa timu na wachezaji kutumia nafasi wanazotengeneza kutafuta ushindi,” amesema Benchikha.

Nahodha wa Simba SC, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, amesema wamerejea nyumbani na wanaelekea kwenye mechi dhidi ya Jwaneng Galaxy kwa tahadhari kubwa kulingana na kuwafahamu wapinzani wao hao.

“Hii ni mechi ngumu sana na muhimu kwa Wanasimba wote kujitokeza uwanjani kwa sababu inatoa hatima yetu ya kwenda kucheza Robo Fainali kwa mara nyingine.

“Tunawakumbuka sana Jwaneng Galaxy kwa kilichotokea Uwanja wa Benjamin Mkapa mwaka 2021, hatutafanya makosa tena na tunahitaji kushinda mechi hiyo, ambayo itatupeleka hatua ya Robo Fainalil, lakini tunataka kulipa kisasi.” amesena nahodha huyo

Chanzo: Dar24
Related Articles: