Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha: Wachezaji wako tayari kutupa ushindi kesho

Benchikha Ushindi.png Kocha mkuu wa kikosi cha Simba Abdelhak Benchikha

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa kikosi cha Simba Abdelhak Benchikha amesema mchezo wao dhidi ya Wydad AC wanahitaji ushindi kwa hali na mali, na ili wapate ushindi lazima wachezaji wake wajitume na wapambane kwani anajua wana huo uwezo.

"Mechi hii ni mhimu kwetu kupata ushindi, ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele hatua inayofuata.

Tunatakiwa kuwa na nguvu ya pamoja na umakini mkubwa, wachezaji wangu wanauwezo wa kulitimiza hili na wanajiamini kwaajili ya kushinda mchezo dhidi ya Wydad AC.

Simba itashuka dimbani kesho katika uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa nne wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Hadi hivi sasa Simba wana alama mbili [2] pekee jambo ambalo linawaweka katika mazingira magumu kwenye msimamo wa kundi wakihitaji zaidi ushindi katika mchezo huu ili warejeshe matumaini ya kufuzu robo fainali.

Wydad AC ina alama tatu [3] ilizozipata baada ya ushindi katika mchezo uliopita dhidi ya Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: