Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchikha: Hao Wydad tunao

Benchikha Morocco.jpeg kocha Abdelhak Benchikha

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuanza mechi za Ligi Kuu Bara kwa kishindo kwa kuifumua Kagera Sugar kwa mabao 3-0, Kocha Abdelhak Benchikha amegeuza makali kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa kesho dhidi ya Wydad AC ya Morocco akiwajaza upepo mastaa wa timu hiyo, iwe isiwe ni lazima washinde Kwa Mkapa.

Simba itaikaribisha Wydad Uwanja wa Benjamin Mkapa, katika mechi ya raundi ya nne ya Kundi B na kocha Benchikha amesema hiyo ni kama fainali kwao, wakifanya uzembe wowote watajiweka pabaya katika mbio za kutaka kwenda robo fainali ya michuano hiyo kwa msimu huu.

Katika mechi ya kwanza iliyopigwa wiki iliyopita, Wydad ilishinda bao 1-0 nyumbani na kuifanya Simba ikae mkiani mwa kundi hilo linaloongozwa na Asec Mimosas ya Ivory Coast, ikifuatiwa na Jwaneng Galaxy ya Botswana kisha Wydad ikifuatia nafasi ya tatu.

Kutokana na hali ilivyo kundini, kocha hiyo mpya kutoka Algeria anapiga hesabu za kutaka kupenya na haiwezi kuwa rahisi kama hawataibuka na ushindi kwenye mchezo huo wa kesho utakaopigwa kuanzia saa 10:00 jioni.

Kocha huyo aliyeiongoza Simba kwenye mechi mbili zilizopita za Caf na kuambulia pointi moja iliyopatikana katika suluhu dhidi ya Jwaneng kabla ya kupasuka Marrakech, Morocco kwa kufanya kikaon na mastaa wa timu hiyuo akiwataka kupambana mwanzo mwisho kuhakikisha wanashinda kabla ya kusubiri mechi mbili zilizosalia.

“Mechi na Wydad inatakiwa kuwa upande wetu, tunahitaji kushinda ili kurejesha matuamini kikosini. Tulipoteza kwao dakika za mwisho lakini tulicheza vizuri, haitoshi kujivunia kucheza vizuri tunachotaka sasa ni alama tatu muhimu na hilo tulifanye kuwa lazima,” amekaririwa Benchikha akizungumza na mastaa wa timu hiyo kambini.

Kocha huyo amewatoa hofu wachezaji na mashabiki wa Simba akiwaeleza Wydad ni timu yenye jina kubwa lakini inafungika na sasa ndio wakati wa Simba kuthibitisha hilo.

“Hakuna timu isiyofungika, tuondoe mawazo hasi kichwani kwetu tutaingia uwanjani tukiwa kifua mbele na lengo likiwa ni kushinda. Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa nguvu timu yao naamini baada ya mechi tutafurahi kwa pamoja,” alisema Benchikha ambaye kabla ya kutua Simba aliwahi kukutana na Wydad mara kadhaa akiwa na timu za Difaa el Jadida, Maoladia na RS Berkane zote za Morocco na katika mechi 10 alipokutana na Wydad alishinda nne, sare mbili na kupoteza nne hivyo anaijua vyema timu hiyo.

Beki wa zamani wa Simba, Boniface Pawasa alisema uwanja wa nyumbani ni silaha moja wapo katika michuano ya kimataifa hivyo Simba inatakiwa kuutumia vyema kuhakikisha inapata alama.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: