Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Benchika aweka kikao cha dharura Azam Complex

Simba Kiko Chamazi.jpeg Benchika aweka kikao cha dharura Azam Complex

Fri, 15 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha Mkuu wa Simba, Abdelhak Benchika ameweka kikao cha dharura na benchi lake la ufundi kilichodumu kwa dakika 12, baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara wa Simba dhidi ya Mashujaa FC kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam, Wekundu wa Msimbazi ikishinda mabao 2-0

Benchikha aliwazuia makocha wote wanne kwa maana ya msaidizi, Farid Zemiti na kocha wa viungo Kamal Boujdjenane na baadae aliongezeka kocha wa makipa Dani Cadena, huku kocha msaidizi namba mbili, Seleman Matola akifanya mahojiano na wanahabari.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye mabenchi ya uwanja huo, Benchikha ndiye alikuwa mzungumzaji mkuu huku wengine wakichangia.

Baada ya mechi ya leo, Simba itaingia chimbo kujiandaa na mechi ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, mtanange utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Machi 29 mwaka huu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: