Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Mtibwa ampa Cadena maua yake

Daniel Cadena Simba.jpeg Kocha wa makipa wa Simba, Daniel Cadena

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa zamani wa Mtibwa Sugar, Salvantory Ntebe amemsifu Kocha wa makipa wa Simba, Daniel Cadena kwa kumbadilisha kipa wa timu hiyo Ally Salim na kutamka wazi, kijana ameiva na amemtaka aendelee kukaza.

Ntebe aliliambia Mwanaspoti anaamini siku moja nyanda huyo atakuwa mmoja wa makipa wakubwa nchini kama ataendelea kufanya vizuri.

Alisema amemfuatilia Salim katika michezo mitano aliyocheza hivi karibuni na kugundua amebadilika kwa kiasi kikubwa na kuwa bora sana tofauti na msimu uliopita alikuwa akifanya makosa ambayo yalisawazishwa na mabeki wake.

“Kijana amebadilika sana, ukimwangalia anavyocheza krosi, penalti na kuokoa mashambulizi, ni wazi amebadilika kwa kiasi kikubwa, amekuwa bora sana, yale makosa ya msimu uliopita ameyarekebisha," alisema Ntebe na kuongeza;

“Sasa anapanga na kuzungumza na mabeki wake, anafanya maamuzi kwa wakati sahihi, kwa kweli kwangu kama akiendelea kujituma basi atapata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza hata kama Aishi Manula atapona na kurudi kikosini."

Hata hivyo, Ntebe alisema sifa za uimara wa kipa huyo zinatakiwa pia ziende kwa kocha wa makipa wa timu hiyo, Cadena ambaye kwake anaona ndiye aliyeweza kumbadilisha kipa huyo na kuondoa kabisa mapungufu yake.

“Lazima tumpe sifa pia huyo kocha mpya wa makipa wa Simba (Cadena), amemweka sawa maana udakaji wake kwa sasa unaona ni wa kufundishwa kabisa, hivyo kama akiendelea kuwa msikivu basi atapata vitu vingi kutoka kwa huyo kocha," alisema beki huyo.

Kuhusu mwenendo wa Ligi Kuu, Ntebe alisema; “Ligi imeanza kwa kasi, naona kabisa kama wakiendelea hivi basi msimu huu haya mashindano yatakuwa na ushindani mkubwa sana jambo linalofanya yawe na upinzani mkubwa."

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: