Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balua: Malengo ya Simba ni nafasi ya pili

Balua Simba Sz Edwin Balua.

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga wa Klabu ya Simba, Edwin Balua amesema kuwa malengo yao kwa sasa ni kushika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya NBC ili wapate nafasi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika.

Balua amesema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa ligi dhidi ya tabora United huku mchezo huo ukimalizika kwa Simba ambao wapo nafasi ya tatu kushinda bao 2-0 na Balua akifunga bao a pili.

“Hamna siri yoyote zaidi ya matumizi ya mwalimu kwa mchezaji husika kama ameona ninaweza kufiti kwenye mfumo wake ndiyo maana unaniona uwanjani. Aina ya mabao ninayofunga ni kutokana na maelekezo ya mwalimu na jitihada zangu pia. Tofauti na mazoezi ya timu ninafanya mazoezi binafsi kwa muda wangu binafsi.

“Malengo yetu makubwa ni kuhakikisha tunaipata nafasi ya pili ili tuendelee kushiriki mashindano ya kimataifa yanayokuja, hilo ndilo muhimu. Mashabiki waendelee kutusapoti wasiichoke timu, wasituache. Sisi tunawategemea wao na wao wanatutegemea sisi,” amesema Balua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: