Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baleke hakuna kulala Simba

Baleke Raja Baleke

Thu, 6 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ likiongozwa na straika, Jean Baleke, juzi Jumapili usiku liliingia kambini kuanza maandalizi ya mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports dhidi ya Ihefu SC.

Hiyo ni baada ya msafara wa Simba kurejea jijini Dar es Salaam ukitokea Morocco ambapo timu hiyo ilikwenda kumalizia mchezo wa mwisho wa Ligi ya Mabingwa Afrika Kundi C na kupoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya Raja Casablanca, lakini tayari imefuzu robo fainali.

Ijumaa ya wiki hii, Simba inatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar kuvaana na Ihefu kuwania nafasi ya kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Akizungumza nasi, Robertinho alisema kikosi hicho kimeingia kambini tayari kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mchezo huo ambao muhimu kwao kupata ushindi.

“Baada ya mapumziko ya siku mbili, kikosi changu kimeingia kambini jana (juzi Jumapili) usiku, kikiwa na wachezaji wote kwa lengo la kupata ushindi dhidi ya Ihefu.

“Mara baada ya timu kuingia kambini, nilifanya kikao na wachezaji wangu wote na kikubwa niliwataka kusahau matokeo ya mchezo dhidi ya Raja Casablanca na badala yake kuuangalia huu wa Ihefu,” alisema Robertinho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: