Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baleke ahakikishe anafunga katika mechi muhimu

Mayele Baleke Dd Baleke ahakikishe anafunga katika mechi muhimu

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika mafanikio makubwa ya klabu ya Yanga misimu iliyopita mpaka kufika fainali katika kombe la shirikisho na kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara mbili mfululizo.

Kwa asilimia kubwa ulitokana na Fiston Mayele, Alikuwa na mwendelezo wa kufunga mabao katika mechi za aina zote iwe na mechi na dhidi ya klabu ndoto na zile mechi kubwa au zinazohitaji sana matokeo mazuri ya ulazima

Baleke anaonekana kufunga mabao mengi katika mechi za kawaida ambazo klabu ya Simba inaweza kupata matokeo hata kama Baleke atakosekana katika mchezo

Kumbuka mchezo wa ugenini dhidi ya Power Dynamos Baleke alipoteza nafasi nyingi ambazo kama angezitumia ipasavyo basi mchezo ungemalizika ugenini kule nchini Zambia

Wote tunatambua ubora Baleke katika kufunga na tunajua anakipaji kikubwa cha ufungaji lakini kwa sasa tunataka tuone anaibeba Simba na anafunga mabao katika mechi ngumu ambazo klabu ya Simba itaweza kutwaa ubingwa wa ligi na kufanya vizuri kimataifa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: