Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baleke, Phiri na Chama watajwa kuimaliza Prisons

Baleke Onana Baleke, Phiri na Chama watajwa kuimaliza Prisons

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Simba ikijiandaa kuwavaa Tanzania Prisons leo Alhamisi saa 10:00 jioni, mashabiki wa timu hiyo wamesema wanahitaji pointi tatu ili kukaa kileleni, huku wakitaja mastaa watakaomaliza mechi hiyo.

Timu hizo zinakutana katika mchezo wa Ligi Kuu raundi ya nne. Ambapo Simba haijapoteza wala kutoa sare mechi yoyote na kuwa nafasi ya tatu kwa pointi tisa, huku Prisons wakiwa mkiani kwa pointi moja.

Rekodi inaonesha mechi 10 za mwisho kukutana wapinzani hao, Simba ameshinda mechi tano, akipoteza miwili na sare tatu japokuwa msimu uliopita Prisons ilipoteza nyumbani na ugenini ikiruhusu jumla ya mabao nane ikifunga moja.

Nelson Abute shabiki wa Wekundu mkoani Songwe, alisema matarajio yao ni kushinda ili kukaa kileleni akiwataja, Luis Miquisone, Clatous Chama na Moses Phiri kumaliza shoo.

“Lazima prisons wafe matatu, Chama, Miquisone na Phiri watamaliza kila kitu, Simba ni timu bora na nina matumaini makubwa na timu yangu kwa ubora walionao,” amesema Steven.

Naye Jankus Steven amesema kutokana na ubora walionao Simba, leo lazima Maafande walale mapema akisema wachezaji Andre Onana, Jean Baleke na Chama akiwapa matumaini kutupia.

“Mashabiki wasiwe na wasiwasi kikosi kipo imara na leo tunamfunga mtu na kukwea kileleni, wachezaji wa kutupa raha ni Baleke, Onana na Chama,” ametamba Steven.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: